Back to top

Mpina aivunja bodi ya wakurugenzi ya Maziwa Tanzania.

22 August 2019
Share

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Mpina ameivunja bodi ya wakurugenzi ya bodi ya maziwa nchini Tanzania kuanzia leo Agosti 22, 2019 kutoka na kutoridhishwa na utendaji wa bodi hiyo.

Mhe.Mpina ameivunja bodi hiyo kwa mamlaka aliyopewa kisheria chini ya bodi ya maziwa No.8 ya mwaka 2014 kifungu cha 8 na 9 (1).