
Mradi wa kuchakata na kusindika gesi asili kuwa kimiminika (LNG) unategemewa kufanya uzalishaji kwa zaidi ya miaka hamsini (50)tangu kuanza uzalishaji na kuleta manufaa makubwa kwa taifa ikiwemo ajira na kuongeza pato la taifa kwa kuingiza fedha za kigeni kupitia uuzaji wa gesi nje ya nchi.
Akiongea kuhusiana suala hilo, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Petroli, Halfani Halfani amesema mradi huo utaleta tija na manufaa makubwa kwa taifa kwa kuleta faida mara mbili kupitia gesi itakayouzwa ndani na nje ya nchi, mradi huo utadumu kwa zaidi ya miaka 50 na kuleta mapinduzi makubwa husani katika kurahisisha upatikanaji wa nishati kwenye viwanda nyumba, magari, ikiwemo taasisi mbalimbali pamoja na kupunguza gharama za uzalishaji nchini.
Hata hivyo Halfani ameongeza kuwa kwenye mradi huo wafanyakazi wasiopungua 500, watapata kazi na kwamba katika eneo hilo la mradi kutakuwa na ajira nyingi kwa watu wa bodaboda, mama ntilie pamoja na wajasiriamali wengine wa aina mbalimbali, huku mamlaka hiyo ikindelea kuhakisha wa zawa sana faidika na miradi ya mafuta na gesi.
Aidha katika hatua nyingine baadhi vijana wa Kitanzania wameipongeza serikali kwa kupitia PURA kuweka mazingira wezesha ya ajira katika sekta ya madini na gesi ambapo kwa upande watumaini Abdallah ni mmoja wa vijana wanaofanyakazi kwenye Kampuni za kizalendo zitakazonufaika na mradi wa LNG, yeye ameipongeza Pura kwa kuziamini kampuni za ndani za uchimbaji wa gesi na mafuta.
