Back to top

Mradi wa SGR wafikia hatua nzuri.

12 December 2019
Share

Mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) yenye mtandao usiopungua Kilomita 2,561 ambao kipande cha kwanza cha Dar Es Salaam - Morogoro kimefikia asilimia zaidi ya 70 na kipande cha Morogoro - Makutupora Singida kimefikia zaidi ya asilimia 20.
 
Mradi huo uliofadhiliwa na serikali ya Tanzania kwa kutumia fedha za ndani kwa asilimia 100.

Kuunganisha mikoa ya Dar Es Salaam, Mwanza, Kigoma, Katavi na nchi zisizokuwa na bandari (Rwanda Burundi na DRC), ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa alibainisha hayo katika utoaji wa taarifa ya miaka 4 ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano katika sekta ya miundombinu ya reli nchini.