Back to top

Msaidizi wa ndani auwa mama na Watoto wake wawili – Dar es salaam.

12 June 2021
Share

Jeshi la polisi limethibitisha kumshikilia kijana mmoja aliyefahamika kwa majina ya Shedrak Kapanga, kwa tuhuma za kumuua bosi wake na Watoto wake wawili kwa kile alichodai kugombezwa mara kwa mara na bosi wake huyo.

Mtuhumiwa huyo alitekeleza tukio hilo mnamo tarehe 09 mwezi wa sita maeneo ya Masaki Dar es Salaam.

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi kanda maalum Dar es Salaam Muliro Jumanne Muliro.