Back to top

Msako mkali madereva wanaotumia vilevi.

10 August 2022
Share

Siku tatu baada ya kutokea ajali iliyosababisha vifo vya watu 20 katika eneo la Mwakata wilayani Kahama, Jeshi la Polisi nchini limetangaza,  oparesheni maalum ya ukaguzi wa madereva walevi, na magari yasiyo na viakisi mwanga, ili kudhibiti ajali za mara kwa mara zinazosababishwa na changamoto hiyo.


Kauli hiyo imetolewa  na Kamanda wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Awadhi Juma Haji, baada ya kuwatembelea majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama.