Back to top

Msando akabidhi milioni 5 gharama anazodaiwa Bi.Sabina Muhimbili.

23 August 2019
Share

Wakili Alberto Msando ameikabidhi hospitali ya Taifa Muhimbili shilingi milioni 5 kwa ajili ya kulipa gharama alizokuwa akidaiwa Bi.Sabina Kitwae ambaye alifiwa na mama yake mzazi hospitalini hapo.

Msando amemkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbil Prof.Lawrence Museru fedha hizo ambazo zimepatikana kupitia michango iliyotolewa na baadhi ya watanzania kupitia uhamasishaji aliofanyika kupitia mtandao wa kijamii (Instagram) ili kulipa gharama alizokuwa akidaiwa mama huyo.

Awali mama huyo alifikisha kilio chake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli alipofika hospitalini hapo kuwajulia hali majeruhi wa moto wa ajali ya lori Morogoro waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Hata hivyo kiasi kilichobaki sasa ni kwa ajili ya kukamilisha deni la mama huyo analodaiwa hospitalini hapo ni zaidi ya shilingi laki 364,814.02 . 

Taarifa zaidi kukujia.