Back to top

MSD YAFIKISHA DAWA NA VIFAA TIBA KATESH

04 December 2023
Share

Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) imefikisha msaada wa dawa na vifaa tiba kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko Hanang katika Hospitali ya Wilaya ya Hanang (Tumaini).


Meneja wa Kanda ya MSD Kilimanjaro Rehema Shelukindo ameeleza kuwa, vifaa hivyo ni pamoja na maji tiba (drips), dawa za kuponya magonjwa ambukizi na mengineyo (antibiotics), dawa za maumivu na mashuka.
.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai ameeleza kuwa MSD itaendelea kupeleka bidhaa za afya katika eneo hilo kadri itajavyoelekezwa na Serikali.