Back to top

Mshambuliaji Texas alituma ujumbe mtandaoni.

26 May 2022
Share

Gavana wa Jimbo la Texas Greg Abbott amesema kuwa mshambuliaji aliyeua watu 21 wakiwemo watoto 19 alituma ujumbe kwenye mtandao wake wa kijamii muda mfupi kabla hajatekeleza tukio hilo katika shule ya Robb Elementary School.

Gavana alisema Ramos aliahidi kumpiga risasi bibi yake katika jumbe za faragha zilizotumwa dakika 30 kabla ya shambulio hilo na ujumbe wa baadaye ulionyesha kwamba alikuwa amefanya hivyo, na katika jumbe ya mwisho aliyotuma dakika 15 kabla ya kushambulia shule hiyo, alitangaza kushambulia shule ya msingi.

Kwa mujibu wa CNN, jumbe hizo za faragha zilitumwa kwa msichana wa miaka 15 nchini Ujerumani ambaye Ramos alikutana naye mtandaoni.