Back to top

MSIGWA: JOACHIM AMEFARIKI KWA AJALI YA BAISKELI

14 December 2022
Share

#UPDATE: Kufuatia kifo cha Mwandishi wa Habari wa Shirika La Utangazaji Tanzania (TBC), Joachim Kapembe, aliyefariki wakati akishuka Mlima Kilimanjaro, Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa ambaye ni mmoja waliopanda nae kwenye mlima huo amesema Kapembe amefariki dunia kwa ajali ya baiskeli wakati akitoka katika kambi ya Kibo kuelekea kambi ya Horombo, baada ya kupanda mlima hadi kufika kileleni kwa mafanikio.
.
Msigwa ameongeza kuwa Kapembe, ni mmoja wa watu ambao hawakupatwa na madhara ya kupanda mlima (mountain sickness) na alifanya kazi yake vizuri ikiwemo kurekodi na kuhoji watu mbalimbali.