
Serikali imewataka wasimamizi wa Afya ngazi ya Mkoa, kuacha tabia ya kuvilazimisha vituo vya kutolea huduma za afya, kununua dawa kwa washitiri ambao wanawataka wao ili kutatua kero ya uhaba wa dawa katika vituo, pindi washitiri hao wanapokuwa na upungufu wa dawa.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, wakati akijibu maswali bungeni Jijini Dodoma, ambapo amewataka wasimamizi hao, kutengeneza biashara huria ili vituo viweze kununua dawa kwa mshitiri yoyote aliyetimiza vigezo.
