Back to top

Msitume SMS ambazo mteja hajaomba - Nape Nnauye

02 June 2022
Share

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye ameziagiza kampuni za simu nchini kuacha mara moja tabia ya kutuma ujumbe (SMS) ambao haujaombwa na Mteja kwani kufanya hivyo ni kuwapotezea muda na ni usumbufu kwa wateja huku akiielekeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kushirikiana na kampuni za simu kusimamia agizo hilo.