
Kufuatia kukithiri kwa vitendo vya kihalifu yakiwemo mauaji katika Mkoa wa Tanga, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe.Hamad Masauni amewataka wananchi kuondoa hofu, kwani Jeshi la Polisi limejizatiti kukabiliana na vitendo hivyo.
.
Masauni ameyasema hayo wakati akiongea na viongozi mbalimbali wa serikali, dini, wawakilishi wa vyama vya siasa na vijana wanaojihusisha na biashara ya kubeba abiria kwa pikpiki (bodaboda) mkoani humo.
