Back to top

Mtangazaji maarufu nchini Marekani Larry King (87), Afariki Dunia.

23 January 2021
Share

Mtangazaji maarufu nchini Marekani Larry King ambaye ana miaka 87, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika kituo cha Cedars-Sinai, huko Los Angeles.

Chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi, mtangazaji huyo ameendesha kipindi cha 'Larry King Live' kwa zaidi ya miaka 25 katika runinga ya CNN kati ya mwaka 1985 na 2010, akihoji watu tofauti tofauti.

Ikumbukwe pia hivi karibuni, King alikuwa anafanya kipindi kingine kingine cha Larry King Now, kupitia mtandao wa Hulu pamoja na kituo cha Televisheni cha kimataifa cha RT kinachomilikiwa na serikali ya Urusi.