Baba adaiwa kumuua kikatili mwanae kwa kumuunguza na moto sehemu mbalimbali za mwili kwa kile kinachodaiwa mtoto kuyo alijisaidia kitandani usiku huko wilayani Ngara mkoani Kagera.
Kamanda wa polisi wa Kagera Revocatus Malimi amesema mtoto Bahati Juma mwenye umri wa miaka miwili alipoteza maisha wakati akikimbizwa hospitali na wasamalia wema na jeshi hilo linamshikilia mtuhumiwa Juma Daniel.