Back to top

Mtoto ampiga risasi mwalimu wake Marekani.

10 January 2023
Share

Polisi nchini Marekani wamesema mtoto wa miaka sita aliyempiga risasi mwalimu wake, katika shule ya Richneck Elementary nchini humo alitumia bastola ya mama yake iliyonunuliwa kihalali, ambapo inadaiwa kuwa alikusudia kumpiga risasi mwalimu wake na awali mtoto huyo waligombana na mwalimu wake.

Mtoto huyo alimpiga risasi mwalimu wake Abigail 'Abby' Zwerner, kwa makusudi wakati wakiwa darasani na bastola hiyo aliyokuwa ameibeba kwenye mkoba wake wa shule. Polisi wanasema mwalimu huyo alifanikiwa kuwaokoa wanafunzi wake wa darasa la kwanza na kuwapeleka hadi mahali salama kabla ya kuomba msaada.