Back to top

Mtoto amuua baba yake na kuuteketeza mwili.

11 September 2020
Share

Polisi nchini Kenya inamsaka kijana wa miaka 20 Michael Muchiri  aliyemuua babake mzazi John Mwangi na kuuteketeza mwili huo kwa mafuta ya petroli huku chanzo kikitajwa kuwa ni mzozo uliokuwepo baina yao.

Taarifa za awali zinasema kijana huyo alikuwa mrahibu wa dawa za kulevya kwa muda mrefu.

Polisi nchini Kenya wanasema  sio mara ya kwanza kwa kijana huyo kuwashambulia jamaa zake huku ikidaiwa kuwa majuma yaliyopita alikuwa ametishia kumkatakata mamake mzazi na mama yake huyo aliokolewa na wanakijiji.