Back to top

Mtoto amuua mama yake kwa shoka Arusha.

16 May 2020
Share

Watu wawili wamepoteza maisha katika matukio mawili tofauti yaliyotokea mkoani Arusha likiwemo la mama aliyekatwa panga na mwanaye na tukio la pili likitokana na ajali ya moto. 

Kamanda wa polisi  wa  mkoa  wa  Arusha Jonathan Shana anaelezea jinsi tukio  la mauaji  lilivyotokea katika kijiji cha Sakila chini wilayani Arumeru ambapo mama mmoja aliyetajwa kwa jina la Eliyamulika Emanuel Sarakikya (79) ameuawa kwa kukatwa na shoka na mtoto  wake aliyetajwa kwa jina la Bw.Daniel  Emanuel.
 
Kamanda Shana pia akaelezea tukio la moto lilitokea eneo la Sanawari katika kata ya Sekei jijini Arusha usiku wa kuamkia 16/05/2020  baada ya duka la bidhaa mbali mbali kuteketea kwa moto huku kijana huyo akiwa ndani amelala.