Back to top

MTOTO ATOLEWA 'SKRUBU' ILIYOKWAMA KWENYE MAPAFU

23 January 2024
Share

Hospitali ya Taifa Muhimbili imefanikiwa kumtoa Mtoto mwingine Skrubu (Screw) kwenye mapafu yake kwa kutumia kifaa chenye kamera.

Mtoto huyo alikuwa akiichezea mdomoni skrubu hiyo, wakati akiwa shuleni na ndipo ikampalia kumpalia na kukwama.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mapafu na Mfumo wa Upumuaji, Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Mwanaada Kilima, amesema mtoto huyo alipaliwa na skurubu hiyo siku nne zilizopita akiwa shuleni ambayo iliingia kwenye mapafu yake na kusababisha kukohoa.

Bw. Msafiri Chatanda, mzazi wa mtoto huyo amewashukuru watoa huduma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa jitihada kubwa waliyofanya tangu alipofikishwa hospitali hapo na kufanikisha kutoa skurubu hiyo.

Katikati ya mwezi huu, Jopo la Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Kifua na Moyo, Mapafu na Mfumo wa Upumuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili lilifanikiwa kuondoa shanga ya plastiki iliyokuwa imekwama katika pafu la kulia la mtoto mwenye umri wa miaka mitano.

Aidha, mapema jana, Daktari wa Magonjwa ya Mapafu na Mfumo wa Upumuaji, Dkt. Hedwiga Swai akishirikiana na wenzake walifanikiwa kumtoa mama mwenye umri wa miaka 53, ganda la pipi kwenye pafu lake la kushoto alilodumu nalo kwa miaka 11 kwa kutumia kifaa maalum chenye kamera kilichopelekwa moja kwa moja hadi lilipo na kulinasa na kisha kulitoa.