Back to top

MTOTO AUNGUA KWA MVUKE AKITIBIWA DEGEDEGE

04 July 2023
Share

Bi.Jalina Liwajila (42), ambaye ni Mganga wa Kienyeji na Mkazi wa Kijiji cha Rutamba, mkoani Lindi, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa kosa la kumchoma moto mgongoni, mwanafunzi wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka 9, kwa madai kuwa, alikuwa akimtibu ugonjwa wa degedege, ndipo alipomlaza kwenye kitanda cha kamba ambacho chini yake aliweka moto ambao juu yake aliweka sufuria ya maji, yenye majani ya dawa ambayo yalitokota, na kuleta mvuke ambao uliomuunguza mtoto huyo.
.
ITV Imezungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, ACP Pili Mande, ambaye amesema kuwa Bado wanamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi.