Back to top

Mtoto wa miaka 12 adaiwa kuuawa katika kijiji cha Lamadi Simiyu.

14 January 2019
Share

Mtoto wa kike wa miaka 12 Milembe Maduhu amekutwa ameuawa kwenye nyumba ambayo haijakamilika katika kijiji cha Lamadi kitongoji cha Lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu,ambapo watu 3 wanashikiliwa kwa mahojiano.

Chanzo cha mauaji bado hazijafahamika huku Mkuu wa wilaya ya Busega Tano Mwera akiwasihi wakazi wa Lamadi kutulia wakati polisi wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.