
Mwili wa mwanaume mmoja ambaye jina lake halijatambulika mara moja, umekutwa ukining'inia kwenye uzio wa mataruma ya reli katika mtaa wa Mwere, Manispaa ya Morogoro, huku ikidaiwa kuwa amejinyonga kwa kamba.
Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kushtushwa na kuingiwa na hofu baada ya kukuta mwili huo pembezoni mwa barabara ya kuelekea stesheni ya reli ya kati, eneo ambalo hutumiwa na wapita njia wengi.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwere, Bw. Mussa Kasita, amethibitisha kutokea kwa mkasa huo na kueleza kuwa tayari Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu.
Mwili huo umehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kitabibu ili kubaini chanzo cha kifo hicho, huku taratibu za kuwatambua ndugu wa marehemu zikiendelea.
