Back to top

Mtu mmoja anatafutwa na polisi kwa tuhuma za mauaji ya mkewe na mtoto.

24 May 2018
Share

Kamanda wa polisi mkoani Tabora Kamishina Msaidizi Mwandamizi Wilbrod Mutafungwa amesema kuwa,katika kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimampenzi,Jeshi hilo linamtafuta mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Omari Matonya baada ya kuwachinja mama na mtoto wake na kisha kutoroka.

Katika hatua Nyingine Jeshi la polisi mkoani Tabora linamshikilia mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Kiwere wilayani Sikonge mkoani humo baada ya kumkamata na silaha nane za moto aina ya magobore ambazo zinasadikiwa kutumika katika kufanya ujangili katika hifadhi ya wanyama wilayani humo.

Kamanda Mtafungwa amemtaja mtu huyo kwa majina ya Ibrahimu Yohana miaka 40,ambaye haikujulikana silaha hiyo zinatumika kwa kazi gani huku akidai upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.