Back to top

MTUHUMIWA UTAPELI VIWANJA AFIKISHWA MAHAKAMANI

08 March 2024
Share

Mtuhumiwa wa wa kutapeli na kudhulumu viwanja vya watu na kujimilikisha kinyume na utaratibu Jijini Dar Es Salaam, Paul Mushi ametolewa kituo cha Polisi Oysterbay na kupelekwa Mahakama ya mwanzo Kinondoni.

Hatua hiyo imefuatia baada ya mtuhumiwa huyo kukamwatwa hapo awali kwa tuhuma za kunyang'anya viwanja vya watu kadhaa na sasa amepekwa Mahakamani ili hatua za kisheria ziendelee.

Hatua hiyo inakuja baada ya  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa, kutangaza kuanza kwa operesheni maalumu ya kudhibiti matapeli wa ardhi katika Jiji la Dar es salaam.

Siku chache zilizopita kulifanyika Kliniki ya Ardhi ya Jijini Dar Es Salaam na kuhitimishwa mnamo tarehe 3 Machi 2024 kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi iliyokuwa inasumbua Jiji la Dar Es Salaam kwa muda mrefu.