Back to top

Mtumbwi watumika kuwavusha wajawazito Korogwe baada ya daraja kukatika

31 March 2020
Share

Wananchi waishio vijiji vya Mabogo,Toronto na Manga Mikocheni  mkoani Tanga hawana mawasiliano ya barabara baada ya daraja linalounganisha vijiji hivyo na cha Mazinde kukatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hali inayowalazimu wakina mama wajawazito pamoja na wanaotoka hospitali kujifungua kupitishwa eneo hilo kwa kutumia mtumbwi.


Kamera ya ITV imeshuhudia mama akivushwa kwa mtumbwi akiwa na mtoto wake mchanga mwenye umri wa siku moja akitokea hospitali kujifungua na mwendesha mtumbwi huo .


Hali hiyo pia imeshuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Kasongwa wakati akiwa kwenye ziara yake ya kukagua ujenzi wa madaraja pamoja na kuwahamisha wananchi kujikinga na ugonjwa wa Corona.