Back to top

Mufti wa Tanzania awataka Waislamu wasibague Elimu.

20 May 2018
Share

Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry amewataka Waislamu nchini kuzingatia elimu kwavile Uislamu haukubali ujinga na Ndio maana hata vitabu vya Dini vinasisitiza elimu ni muhimu bila kubagua ni elimu ya aina gani.

Mufti Abubakary Zubeiry ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waislamu wa kituo cha Masjid Quba Mwanalugali Kibaha katika maadhimisho ya mafunzo maalum yaliyotimiza miaka kumi ya kielimu walengwa wakiwa ni wanawake wa Kibaha na mkoa wa
Pwani.

Kwa upande wake Kaimu Sheikh Mkuu wa mkoa wa Pwani ambaye ni Kadhi mkuu wa mkoa huo Sheikh HamisiAabbas Mtupa amesema zaidi ya wanawake 3000 wamenufaika na programu ya mafunzo mbalimbali ikiwemo mihadhara,malezi ya watoto mahusiano mema kati ya Dini zote amani ndani ya familia na taifa ujumla na elimu inayohusu afya kwa ujumla.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaji Majid Mwanga akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Pwani aliwahkikishia waislamu kuwa mahitaji yote ya waislamu wakati wa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo bidhaa ya mafuta,futari vinapatikana kwa
Kama kawaida na kwa bei nafuu.