Back to top

Mugabe kuzikwa Septemba 15, Familia yavutana na serikali.

09 September 2019
Share

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe anatarajiwa kuzikwa Jumapili, Septemba 15, baada ya sherehe rasmi itakayofanyika Jumamosi.

Hata hivyo familia ya Mugabe haijakubaliana na serikali sehemu ambapo atazikwa kiongozi huyo wa zamani wa Zimbabwe.

Mwili wake utarejeshwa nyumbani keshokutwa kutoka Singapore.

Akizungumza na waandishi wa habari, mpwa wa wa marehemu Bwana Leo Mugabe amesema tangu kiongozi huyo alipoondolewa madarakani shujaa huyo wa zamani wa uhuru, hali yake ya afya iliendelea kudhoofika.

Hata hivyo hajui mjomba wake alitaka azikwe wapi, lakini anaamini mazishi yatafanyika katika makaburi ya Mashujaa wa Taifa, kama ilivyopangwa kabla ya kutimuliwa kwake madarakani.