Back to top

MUHIMBILI KUJENGA HOSTELI ZA NDUGU WA WAGONJWA

17 May 2024
Share

Serikali imesema tayari Hospitali ya Taifa Muhimbili imeandaa mpango wa uendelezaji wa eneo la Hospitali hiyo, ambapo mojawapo ya maeneo yatakayokuwepo kwenye mpango huo ni kujenga hosteli za bei nafuu ambazo ndugu wa wagonjwa watakaa.
.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Hawa Mwaifunga, aliyeuliza, ni lini Serikali itatenga eneo maalum katika hospitali za Muhimbili na MOI kwa ajili ya watu wasio na ndugu Dar es Salaam wanaopeleka wagonjwa kupata matibabu?.
.
Dkt. Mollel ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2024/25 Hospitali ya MOI imeandaa mpango wa mashirikiano na sekta binafsi ili ndugu wasio na mahala pa kulala toka ndani na nje ya nchi waweze kupokelewa katika hosteli zilizo karibu na Muhimbili kwa gharama nafuu.