Back to top

MUHOOZI KAINERUGABA KUGOMBEA URAIS 2026

16 March 2023
Share

Mtoto wa kiume wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba,amesema  atagombea urais nchini humo mwaka 2026.

"Katika jina la Yesu Kristo, kwa jina la Vijana wa Uganda na Dunia kwa ujumla na katika jina la Mapinduzi makubwa nitagombea Urais mwaka 2026"- Muhoozi

Mara kadhaa Jenerali Muhoozi amekuwa akiibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kauli zake, ametoa tangazo hilo ametoa kwenye ujumbe wake wa Twitter, akikieleza kuwa watu wamekuwa wakimtaka atoe tangazo hilo.