Back to top

Mume afariki ,mke mahututi wakijaribu kujitibu Corona Marekani.

24 March 2020
Share

Mwanaume mmoja makzi wa Phoenix nchini Marekani amefariki na mkewe yuko mahututi baada ya wawili hao kunywa ‘chloroquine phosphate’ wakijaribu kujitibu virusi vya Corona,kwa mujibu wa hospitali ya Banner Health nchini humo.

Licha ya hofu iliyojengeka juu ya ugonjwa wa Corona watalamu wa hospitali ya Banner Health nchini Marekani wamesisistiza kuwa dawa hiyo na dawa zingine ambazo hazijathibitishwa zisitumike kujaribu kujitibu au kujikinga na Corona.