Back to top

Museveni akiri kufungia mitandao ya kijamii nchini Uganda.

13 January 2021
Share

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amethibitisha kuagiza mitandao kadhaa ya kijamii nchini humo kufungiwa.

Katika hotuba yake iliyoonyeshwa mubashara katika televisheni usiku wa Jumanne saa tatu kabla ya muda wa mwisho wa kufanya kampeni, Rais Museveni aliyekuwa amevalia koti la kijeshi alisema ameagiza kufungwa kwa mtandao wa kijamii wa Facebook kwa kuwa na kiburi na kupendelea upande mmoja.

Alisema ikiwa Facebook itatumiwa nchini Uganda, lazima itumiwe kwa usawa na kila mtu anayetaka kufanya hivyo. Museveni pia alisema hatakubali mtu yeyote kucheza na nchi yake ama kuamua ni nani mzuri au mbaya.

BBC Swahili