Back to top

Museveni ametangaza mipaka yake itaendelea kufunguliwa.

19 May 2020
Share

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza  mipaka yake itaendelea kufunguliwa,akidai kwamba hawezi kusukumwa na hasira za raia kuifunga kwa kisingizio cha homa ya COVID19.

Museveni anasema kwamba asilimia kubwa ya uchumi wa taifa lake hutegemea usafirishaji mizigo kutoka bandari kuu ya Mombasa na Tanga,na kwamba hakuna haja ya kulinyonga taifa lake kiuchumi kwa  zoezi hilo.

Badala yake ameamrisha kwamba madereva wote wapimwe mipakani kabla ya kuruhusiwa kuendelea na safari,wanaobainika wakiruhusiwa kurejea nyumbani kwa matibabu.

Maamuzi ya Museveni yametolewa baada ya Kenya kuamua kufunga mipaka na Tanzania na Somalia.