Back to top

Museveni aongoza matokeo ya awali nchini Uganda.

15 January 2021
Share

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais uliofanyika jana nchini Uganda yaliyotolewa usiku wa kuamkia leo yanaonesha rais Yoweri Museveni anaongoza dhidi ya mpinzani wake mkuu Robert Kyagulanyi.

Kulingana na Tume ya Uchaguzi nchini humo matokeo ya awali kutoka vituo visipungua 300 vya kupigia kura, yanaonesha rais Museveni wa tawala cha NRM amepata asilimia 61.3 huku Kyagulanyi maarufu Bobi Wine kutoka chama cha NUP amejikingia asilimia 27.9 ya kura.

DW