Back to top

Muuguzi kizimbani kwa kupokea rushwa ya elfu 20 kwa ndugu wa mgonjwa.

22 January 2020
Share

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Lindi,itamfikisha  mahakamani muuguzi wa hospitali ya wilaya ya Ruangwa,Bi. Nasra Ally Mandamba, kwa tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa ya shilingi elfu 20 kutoka kwa ndugu wa mgonjwa  aliyekuwa amelazwa hospitalini hapo kwa ajili ya kujifungua.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Lindi Bw.Stephen Chami, ofisini kwake wakati anatoa taarifa ya robo ya mwaka  mbele ya waandishi wa habari.