Baraza la uuguzi na ukunga nchini limemsimamisha kazi muuguzi wa hospitali ya Mount Meru Bwana Martin Chamani kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa kosa la kuingia kazini akiwa amelewa kinyume na maadili na kanuni za utumishi.
Akizungumza jijini Arusha Mwenyekiti wa baraza hilo Abner Mathube anasema licha ya kukiuka maadili ya taaluma ya uuguzi, ulevi kazini unahatarisha maisha ya wagonjwa.