Back to top

MV Magogoni yapata hitilafu - TEMESA

02 June 2022
Share

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) imetoa taarifa kwa umma kuwa Kivuko cha MV Magogoni kinachotoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni kimeshindwa kutoa huduma leo asubuhi Juni 02, 2022 baada ya kupata hitilafu hivyo kusababisha huduma kusimama kwa muda huku shughuli za uvushaji abiria zikiendelea kwa kutumia kivuko cha MV. Kigamboni.
.
Hata hivyo TEMESA wamebainisha kuwa mafundi wanaendelea na zoezi la marekebisho ili kuweza kurudisha huduma za kivuko hicho haraka iwezekanavyo.