Back to top

Mvua Mtwara: Familia 39 zakosa Makazi.

14 January 2021
Share

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara  Gelasius Byakanwa amesema nyumba 315 zimeathirika na maji ya mvua huku watu 39 wakikosa makazi kutokana na nyumba zao kubomoka.
.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa mkoa amesema tayari juhudi mbalimbali zinaendelea kufanyika ikiwemo kuzibua mitaro ili kuruhusu maji kuondoka katika maeneo yaliyoathirika.
.
Baadhi ya watu ambao wamepatwa na majanga ya kubomokewa nyumba na kuzingirwa na maji ya mvua bado wanahifadhiwa katika maeneo yaliyoainishwa na manispaa  zikiwemo shule za msingi na sekondari.

Amesema kwa mujibu wa taarifa za Mamlaka ya hali ya hewa mvua bado ni nyingi hivyo amewataka wakazi wanaoishi mabondeni kuendelea kuchukua taadhari ikiwemo  kuhama maeneo hayo ili kuondokana na madhara yanayoweza kuyakumba.

Mpaka sasa kifo kilichotokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani mtwara ni kimoja.