Back to top

Mvua ya Mawe yasababisha maafa Songwe.

07 November 2019
Share

Mvua ya mawe iliyoambatana na upepo mkali imeezua nyumba ambazo idadi yake bado haijafahamika katika vijiji vya Ihanda na Majengo katika kata ya Ihanda wilaya ya Mbozi mkoani Songwe ambapo mbali ya kusababisha kaya kadhaa kukosa hifadhi, mvua hiyo pia imeharibu mazao ya akiba ya chakula.