Back to top

Mvua yakwamisha zoezi la chanjo mkoani Geita.

18 October 2019
Share

Serikali mkoani Geita imelazimika kuhamishia zoezi la chanjo ya Polio katika maeneo ya ofisi za serikali za  kila vijiji na shule zote ili kuwawezesha wananchi kupata huduma hiyo karibu  kutokana na idadi kubwa ya wanachi kukwama kwenda kupata chanjo hiyo kwa siku mbili mfululizo kutokana na mvua kubwa kuendelea kunyesha.

Akizungumza katika uzinduzi wa zoezi la chanjo kimkoa katika eneo la Nzera mganga mkuu wa wilaya Deo Donard anasema mamia ya wananchi wamekwama kutokana na mazingira ya maeneo ya pembezoni hivyo wameamua kuwafuata walipo

Mganga mkuu wa mkoa wa Geita Dkt.Japheti Simeo  anasema wamelenga kuwafikia watoto zaidi ya laki nne huku akiwataka wananchi kujitokeza katika maeneo ambayo yametengwa karibu ili wapate huduma hiyo

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel anasema mkoa una dawa za kutosha kuwafikia watoto wote akiwaonya wapotoshaji wa chanjo hiyo huku wananchi waliojitokeza wakielezea umuhimu wa chanjo hiyo