Watu watano wamekufa huku kaya zaidi ya kaya 400 kata ya Kisaka wilaya ya Serengeti zikihofia kukubwa na tatizo la ukosefu wa chakula kutokana na mazao yao kusombwa na maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoa wa Mara.
ITV imefunga safari hadi eneo la tukio na kushuhudia mazao yakiwa yameharibiwa na baadhi ya wananchi wakiosha na kuanika mazao yaliyosalia hususani mahindi.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Serengeti ,Nurdini Babu amesema mbali na kuharibiwa kwa mazao pia mvua hizo zimesababisha vifo vya watu watano ambao wamekufa baada ya kusombwa na maji huku akidai serikali inafanya tathimini ili kujua ni hekari ngapi za mazao zimeathirika.