Back to top

Mvua yaua watatu,yakata mawasiliano Songwe, Rukwa na Katavi

11 January 2020
Share

Mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa Rukwa,zimeendelea kusababisha maafa baada ya kusomba madaraja manne katika barabara kuu ya Kasansa-Kilyamatundu inayounganisha mikoa ya Songwe, Rukwa na Katavi iliyopo bonde la ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga huku ikisababisha vifo vya watu watatu katika wilaya ya Kalambo na Nkasi mkoani humo.

Mvua hizo zimesomba madaraja katika vijiji vya Muze, Kifinga, Lwanji na Msia vilivyopo wilaya ya Sumbawanga na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya kata na kata, kijiji na kijiji pamoja na mikoa hali iliyoleta taharuki kwa wananchi wanaoishi katika bonde hilo lenye kata 13.

Kwa upande wake Meneja wa TANROADS mkoa wa Rukwa Mhandisi Masuka Mkina amesemam tayari wamekwisha omba fedha za matengenezo ya Dharula.
Hali hiyo imepelekea mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo  kutembelea maeneo yote yaliokumbwa  na maafa hayo  na kuwatahadharisha wananchi kuacha tabia ya kulazimisha kupita sehemu  zenye  mafuriko.

Barabara hiyo ya Kasansa-Kilyamatundu yenye urefu wa kilomita 178  ni kiungo muhimu kwa kuunganisha mkoa wa Rukwa na mikoa ya Songwe na Katavi hasa katika shughuli za kiuchumi.