Back to top

Mvua yaua watu wa tano mkoani Mbeya, Polisi wathibitisha.

07 October 2019
Share

Watu watano kati yao watoto watatu wamefariki kwa kutumbukia mtoni huku wengine wakisombwa na maji kutokana na mvua zinazoendelka kunyesha mkoani Mbeya.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Ulrich Matei akizungumza na ITV amesema bado wapo katika maeneo hayo kuangalia athari zilizojitokeza kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ofisi ya mkuu wa mkoa.

Amesema katika kuahakikisha taarifa sahihi zinapatikana juu ya madhara ya tukio hilo wameandaa kikosi kazi cha maafa kuzunguka nyumba hadi nyumba Kujua kinachoendelea na madhara yaliyojitokeza.

Aidha Kamanda Matei amesema kuwa kwa sasa pia kinachoendelea ni ukarabati wa Miundombinu iliyoharibika na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya wakazi huku akitoa wito kwa wananchi kuwa na subira kipindi hiki na kuchukua tahadhari katika mito na vivuko wanavyopita.