Back to top

Mvua zasababisha kifo cha mtu mmoja Arusha

09 April 2018
Share

Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Arusha  zimesababisha kifo cha mtu  mmoja  katika  eneo  la  Majengo  huku pia  zikiharibu  miundombinu, na mali  za  wananchi hasa  wanaoishi kwenye maeneo ya Bondeni  na kwenye  mikondo  ya maji  baada  ya  nyumba  zao  kujaa maji.

ITV  imeshudia  Polisi  wakiondoa  mwili  wa  mtu  huyo  kwenye eneo la tukio  huku wananchi  wa mtaa  huo  wa  majengo  wamesema  mtu  huyo  ambaye  ni  mwanamke  na jina  lake halijafahamika  wamemuona  akielea  kwenye Mtaro wa maji nje ya nyumba zao.

Viongozi  wa  eneo  hilo  wamelalamika  kuwa   maji  yanayoingia  kwenye  nyumba zao  ni  matokeo  ya  ujenzi  wa  miunodombinu  ya  barabara  na  wamewalaumu  wakandarasi  kwa kuelekeza  maji kwenye  makazi  yao.  

Hata  hivyo  meneja  wa  wakala  wa  barabara  TANROAD  mkoa  wa  Arusha Bw. John Kalupale pamoja  na  kukiri  kupokea  malalamiko  ya  wananchi  kuhusu  mitaro  ya  maji  kila  mvua  zinaponyesha  amesema  changamoto  kubwa  ni  kuzibwa  kwa  mikondo  ya  maji  kunakotokana  na shughuli  za  binadamu   na  kwamba  wanaendelea  kuzitatua  zilizoko ndani  ya  uwezo  wao   na  zingine  zinaendelea kutatuliwa  na  ngazi  za  utawala 

Bw. Kalupale  amesema pia  lipo  tatizo  la  wananchi  kugeuza  mitaro  ya maji  kama  madampo  ya  kutupa takataka  linalochangia  mitaro  kuziba  na maji  kupoteza  mwelekeo  na  kuingia  kweye  nyumba za  watu.

Jitihada  za  kuwapata   mkurugenzi   wa  jiji   na  mkuu  wa  wilaya  ya Aarusha kuelezea  hatua  za  kiutendaji   na  kiutawala  zinaochukuliwa  kukabiliana  na  changamoto  zinalalamikiwa  zinaendelea   baada  ya  kudai  kuwa   wanatembelea   maeneo   husika  na  watatoa taarifa  baadaye.