
Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Tabora zimekuwa ni changamoto kwa wakulima wa Pamba, kutokana na kutozingatia mda halisi wa kuua wadudu wa zao hilo la biashara, wamekuwa wakilalamikia dawa kuwa haiui wadudu, hali iliyopelekea mkuu wa mkoa kuaza zoezi la uelimishaji juu ya matumizi bora ya dawa.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri katika zoezi la kuwaelimisha wananchi juu ya upuliziaji bora wa dawa katika mashamba ya Pamba, na mda halisi ambapo amewambia wakulima kuwa, watambue hawatazingatia mda wa kupulizia dawa, na ni wakati gani mvua zimenyesha, lengo lililokusudiwa linaweza lisifikiwe.
Aidha katika hatua nyingine amewaagiza wananchi katika halmashauri zenye wakulima wa Pamba, kutowatumia watoto katika kazi ya kupulizia wadudu kuhakikisha wanatumia mda kuwaelimisha wakulima, juu ya manufaa ya zao hilo mbadala wa Tumbaku.
Mkurugenzi wa maendeleo ya watoto wizara ya afya Bibi. Magrethy Mussai, ametawaka wakulima hao kuwapa fursa za kusoma watoto wa kike, na kutambua changamoto ya kitowasomesha na kuwapa kazi ngumu za mashambani akiwataka kuwasomesha kwa manufaa ya familia zao.