Back to top

Mwaisabila apambana na chui na kumuua Mkoani Ruvuma.

04 November 2018
Share

Mkaziwa Kijiji cha Mbesa Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma Bw.Abdala Mwaisabila amepambana na chui na kufanikiwa kumuua.

Kijana huyo alipambana na Chui Huyo baada ya kuvamiwa wakati akiandaa Shamba Kwa ajili ya Msimu wa kilimo wa 2018.

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Misheni ya Mbesa Dkt.Mzelipa Masaaga, Bw.Abdala Mwaisabila ana majeraha saba ya mikwaruzo ya kucha za chui kwenye mkono wakulia na kwamba anaendelea vizuri.