Back to top

Mwakinyo kukipiga na Bondia wa Congo Agosti 14.

09 July 2020
Share

Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo anatarajia kupanda ulingoni Agosti 14 mwaka huu kumenyana na Bondia kutoka DRC ya Congo Tshibangu Kayembe.

Pambano hilo la aina yake la kuwania ubingwa wa WBF linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani city ambapo mabondia hao watapambana raundi 12.

Akizungunzia mtanange huo Mwakinyo amesema yuko tayari kwa pambano hilo kwani amejiandaa vya kutosha kuhakikisha anamaliza pambano hilo mapema na kumuomba rais Magufuli kumuuga mkono 

Aidha Mwakinyo alimuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuri kuunga mkono jitihada za mabondia hapa nchini kama ambavyo amefanya mambo makubwa katika kuendeleza  nchi na jina lake kuzidi kuwa kubwa.

Kwa upande wake Mratibu wa matukio kuelekea pambano hilo Beautrice Said amesema katika pambano hilo kutakuwa na mapambano ya utangulizi nane ya utangulizi ambayo yatawakitanisha mabondia wa hapa Tanzania.

Mwakinyo amepambana mapambano 18 na kupoteza mawili huku mpinzani wake Kayembe amecheza mapambano 12 kashinda 9 na kutoka sare 3.