Back to top

Mwalimu mstaafu aangua kilio baada ya kurejeshewa mil 20 na TAKUKURU.

03 July 2020
Share

Mwalimu Mstaafu Loth Isaac ameangua kilio mara  baada ya kurejeshewa kiasi cha fedha cha milioni 20 na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Manyara zinazotokana na mikopo kandamizi  ambapo alitozwa riba ya asilimia mia tatu na kulazimika kulipa milioni arobaini na mbili baada ya kukopa milioni kumi na nne.

Fedha hizo zimekabidhiwa na Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Bw.Holle Makungu.

Akitoa taarifa ya Utendaji ya TAKUKURU kuanzia mwenzi April mpaka June,mkuu huyo wa TAKUKURU mkoani Manyara amesema kuwa zaidi ya milioni 140 zilikuwa katika mikono ya watu ambao si waaminifu.

Kwa upande wake Mwalimu huyo mstaafu ameishukuru TAKUKURU na serikali ya awamu ya tano kwa kufanikisha kurudisha fedha hizo ambazo alishazipoteza.