Back to top

Mwalimu mtegoni kwa kumuomba rushwa ya ngono mwanafunzi ili ampe cheti

15 December 2019
Share

Mkuu wa shule ya sekondari Serengeti Mwalimu Baraka Sabi amekamatwa jijini Dodoma kwa tuhuma za rushwa ya ngono kwa madai ya kumtaka kimapenzi mwanafunzi aliyemaliza kidato cha sita katika shule hiyo ili ampatie cheti chake cha kumaliza shule.

Akizungumza jijini Dodoma Kamanda Wa Takukuru mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo amesema kuwa walimkamata Mwalimu huyo kwa kushirikiana na mwanafunzi huyo kwa kuweka mtego na kufanikiwa kumkamata Mwalimu huyo akiwa chumbani.