Back to top

Mwanachuo anusurika kipigo, alitupa kichanga

20 June 2022
Share

Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine kilichopo mkoani Mwanza amenusurika kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali baada ya wananchi hao kumtuhumu mwanafunzi huyo kujifungua mtoto kisha kumtupa nyuma ya nyumba anayoishi.
.
Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Silivini ambapo anaishi mwanafunzi huyo wamesema walibaini mwanafunzi huyo kufanya tukio hilo baada ya kugundua uwepo wa damu nyingi kwenye makazi ya mwanafunzi huyo.
.
Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo Mwenyekiti wa Mtaa huo Rajab Ramadhan amesema tayari mwanafunzi huyo amekamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi huku akitoa wito kwa wakazi wa mtaa huo kutoa ushirikiano pindi wanapobaini kuwepo kwa matukio ya kihalifu.