Back to top

Mwanafunzi agoma kwenda kidato cha kwanza kwa madai kuwa hana akili.

16 January 2020
Share

Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15 jina tunalihifadhi aliyefaulu kwenda kidato cha kwanza kwa wastani C katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu wilaya ya Musoma mkoa wa Mara amegoma kwenda shule kwa kile anachodai hana akili ya kusoma masomo ya sekondari huku akitamka mbele ya mkuu wa wilaya kuwa yuko tayari kufungwa na si kusoma.

Akizungumza na ITV akiwa nyumbani kwao mwanafunzi huo amesema alifanya mtihani wa darasa la saba mwaka jana vibaya ili asifaulu lakini anashangazwa na matokeo yanayoonyesha  amefaulu na kudai hayuko tayari kusoma huku akiomba akajifunze kushona cherehani kwani anataka kuwa mwanamitindo

ITV imewatafuta wazazi wa binti huyo na kuzungmza nao ambapo wamesema wamesikitishwa na uamuzi wa mtoto wao na kudai kuwa binti yao ametoweka  kusikojulikana  tangu tarehe 25 mwaka jana na kumtafuta kila mahali lakini baada ya mkuu wa wilaya juzi kutangaza kuwakamata na kuwafunga wazazi ambao watoto wao hawajaripoti shule ndipo  mwanafunzi huyo alipoibuka na kuwataka wazazi wake wampeleke kwa mkuu wa wilaya ili akamueleze kuwa hataki kusoma.