Back to top

Mwanafunzi agongwa na lori, wafunga barabara

30 March 2022
Share

Wananchi wa eneo la Mwatulole lililopo Kata ya Buhalahala mkoani Geita wamefunga barabara kwa mawe wakiitaka serikali kuweka matuta na alama za zebra kwenye eneo hilo baada ya Mwanafunzi wa shule ya msingi Nguzo Mbili aliyejulikana kwa jina la John Frank (7) darasa la kwanza kugongwa na lori na kufariki palepale wakati akivuka barabara kuelekea shuleni.